KIKOSI CHA NAMUNGO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA |
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeipiga faini ya Sh 500,000, Klabu ya Namungo FC ya Lindi kwa kila mechi ambayo mchezaji Imani Vamwanga aliichezea timu hiyo akitumia jina la Emmanuel T. Mwanga katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL), kituo cha Morogoro 2015/2016.
Katika kikao kilichoketi Julai 14, 2016 kujadilina, kupitia, malalamiko na taarifa za waamuzi na Kamisaa za mashindano ya RCL katika kituo cha Morogoro, kamati imebaini kwamba Namungo ilifanya udanganyifu wa jina la mchezaji kwa kumsajili na kumchezesha mchezaji Imani Vamwanga leseni Na. 930909003 ya usajili wa Ligi Daraja la Kwanza FDL msimu wa 2015/2016 klabu ya Kurugenzi Mafinga akitumia jina la Emmanuel T. Mwanga.
Kamati imebaini hayo kupitia taarifa za usajili, ripoti za waamuzi na makamisaa kwa michezo ambayo mchezaji tajwa hapo juu amecheza katika Mashindano ya Ligi ya mkoa wa Lindi na Mashindano ya Ligi ya Daraja la Kwanza FDL msimu wa 2015/16. Namungo inaadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 39 (1) inayozungumza adhabu kwa klabu.
Kamati ya Mashindano ya TFF imetoa uamuzi huo kwa Namungo FC kupigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kila mechi ambayo mchezaji Imani Vamwanga akitumia jina la Emmanuel T. Mwanga amecheza katika mashindano ya RCL.
Pamoja na faini hiyo kwa kila mchezo ambao Namungo ilimchezesha mcheza huyo, timu hiyo Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeitangaza Namungo FC kupanda daraja kwenda Ligi Daraja la pili msimu wa 2016/2017 kama ilivyoainishwa kwenye kanuni ya 5 kipengere cha (4).
Kamati imejiridhisha kwa kupitia taarifa za usajili, ripoti za waamuzi na makamisaa kwa michezo ambayo ilikuwa inalalamikiwa imefikia uamuzi huo kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo. Kamati imeipongeza na kukutakia kila la heri katika michezo.
0 COMMENTS:
Post a Comment