July 20, 2016Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa madawati 200 ikiwa ni sehemu ya mapato ya Ngao ya Hisani utakaochezwa Agosti 17, 2016.

Katika mechi hiyo, Mabingwa watetezi Yanga wataumana na walioshika nafasi ya pili, Azam FC. Hata hivyo, haijajulikana kama TFF ina uhakika wa kupata fedha hizo za madawati kwa uamuzi wake wa kutangaza kutoa hata kabla ya mechi yenyewe.

TFF inaunga mkono juhudi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na juhudi za Serikali kwa ujumla katika kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanakuwa na mazingira bora ya kupata elimu.

Kadhalika TFF inamshukuru Katibu Mkuu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah kwa juhudi za kuendelezaa mpira wa miguu na kuutumia katika kuliletea Taifa maendeleo.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania litaendelea kushirikiana na Ofisi ya Bunge Sports Club katika kufanikisha mashindano mbalimbali hasa mhezo wa Hisani kati ya Simba Sports Club na Young African (Wabunge) utakaofanyika hapo baadaye kwa mujibu wa ratiba na uratibu wa Bunge.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV