July 14, 2016


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema kama wachezaji wake watajiamini, hakuna kitakachowazuia kushinda dhidi ya Medeama, Jumamosi.

Medeama ya Ghana tayari iko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Ghana.

Lakini Pluijm anaamini, kujiamini na kufanya kilicho sahihi, hasa kuzitumia nafasi watakazozipata, ni muhimu sana.

“Kama unapata nafasi, hautumi. Mwenzako akipata anatumia baada ya hapo umekwisha. Nataka wachezaji wajiamini na kufanya kitu sahihi,” alisema Pluijm.
Yanga wamekuwa wakiendelea na mazoezi yao kwenye Uwanja wa Boko Veterani kujiandaa na mechi hiyo.


Yanga wanalazimika kushinda mechi hiyo ili kuinua matumaini yao ya kufanya vizuri katika michuano hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV