July 14, 2016Wapinzani wa Yanga, kikosi cha Medeama ya Ghana, wapo jijini Dar es Salaam.

Medeama wametua kwa makundi kwa kuwa kundi la kwanza limefika leo saa 6:30 mchana na kundi la watu 10 litawasili kesho.


Wenyewe wamesema wapo tayari kwa ajili ya kuwavaa Yanga katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Medeama wana pointi moja baada ya mechi mbili, wako katika nafasi ya tatu. Yanga ndiyo wanashika mkia kwa kuwa hawana pointi hata moja na wanalazimika kuwafunga Waghana hao ili kuchukua nafasi ya tatu.

Nafasi ya pili, wanaishikilia Mo Bejaia wenye pointi nne, TP Mazembe ni vinara wakiwa na pointi sita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV