July 14, 2016

WACHEZAJI SIMBA WAKIMSIKILIZA OMOG BAADA YA MAZOEZI.
Mwendo wa wachezaji wa Simba walio kambini Morogoro umeonyesha kumfurahisha Kocha mpya, Joseph Omog.

Omog anaonekana kufurahishwa na namna wachezaji wake wanavyoyashika mazoezi lakini pia wanavyojituma.

Mmoja wa walio kambini Morogoro, ameiambia SALEHJEMBE kuwa baada ya mazoezi kocha amewaeleza kufurahishwa na hilo.

“Kwa kweli amefurahi sana, ni kweli watu wanajituma naye amesema hilo ameliona na kusisitiza lazima tuendelee kufanya hivyo,” kilisema chanzo hicho.


Simba inaendelea kujiandaa na msimu mpya chini ya Omog ambaye anaonekana kuwa tegemeo kuu la Wanasimba ili kikosi chao kirejee katika enzi zake baada ya kwenda misimu minne bila ya kutwaa kombe la Tanzania Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV