MEDEAMA |
Baada ya suluhu waliyoyapata wapinzani wao wa Kombe la Shirikisho, MO Bejaia na Medeama yamempa matumaini Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Matokeo hayo yamekuja siku moja baada ya Yanga kufungwa bao 1-0 na TP Mazembe na hivyo kushika mkia katika Kundi A la Kombe la Shirikisho.
MO Bejaia na Medeama zilivaana juzi Jumatano nchini Ghana na hivyo kufanya kundi hilo kuwa ngumu.
PLUIJM |
Pluijm amesema suluhu imerejesha matumaini, hivyo alichokipanga ni kushinda michezo yote minne iliyosalia ili hesabu zao ziende sawa.
Pluijm ameongeza kuwa maombi yake katika mchezo huo wa wapinzani ilikuwa ni sare na ndicho kilichotokea.
Aliongeza kuwa, hivi sasa anaendelea kukiboresha kikosi chake kwa kuziimarisha sehemu zenye upungufu ikiwemo safu ya kiungo na ushambuliaji kuhakikisha wanachukua pointi zote zilizobaki kwa ushindi.
"Siku zote wapinzani wako wanapofanya vibaya ni lazima kocha ufurahie kama ilivyokuwa kwa MO Bejaia na Medeama wenyewe wametoka suluhu, ni matokeo tuliyokuwa tunayahitaji ili hesabu zetu ziende sawa.
“Kama nilivyokwambia hivi sasa tunakwenda kimahesabu ili tufuzu kwenye hatua ya nusu fainali nyingine na hilo litawezekana kama na sisi tutashinda michezo mingine ijayo ya nyumbani na ugenini.
"Hivyo hatutakiwi kubweteka na badala yake ni kukiandaa kikosi changu vizuri kuhakikisha tunafikia malengo yetu," alisema Pluijm.
TP Mazembe inaongoza Kundi A ikiwa na pointi 6 baada ya ushindi dhidi ya Medeama wa mabao 3-1 kabla ya kuichapa Yanga bao 1-0.
Mo Bejaia inafuatia ikiwa na pointi nne baada ya kuifunga Yanga bao 1-0 na baadaye sare ya leo. Sasa wana pointi nne katika nafasi ya pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment