July 2, 2016


Serengeti Boys haitaki mchezo, sasa itacheza mechi mbili za mwisho dhidi ya Afrika Kusini na kama itashinda, moja kwa moja itasonga kucheza Kombe la Mataifa Afrika ya vijana chini ya miaka 17.

Katika mechi ya leo, Serengeti imeivurumisha Shelisheli ikiwa kwao jijini Victoria kwa mabao 6-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 9-0 baada ya ushindi wa 3-0 jijini Dar es Salaam.

Hadi mapumziko, kikosi cha Serengeti Boys kinachowavaa Shelisheli kilikuwa kinaongoza kwa mabao 2-0, kabla ya kuongeza mengine manne kipindi cha pili.


Mabao ya Serengeti yamefungwa na Asad Ali katika dakika ta 9 tu na Mohammed Abdallah aliyeachia mkwaju wa nguvu katika dakika ya 43.

Kipindi cha Hassan Juma akaandika bao la tatu kabla ya Issa Juma hajafunga mengine mawili na Yohanna Mkomola akamaliza kazi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV