BEKI wa kati wa Yanga, Bakari Mwamnyeto ambaye ni mzawa, amempoteza mazima beki kisiki wa Simba, Joash Onyango raia wa Uganda kwenye kazi ya ulinzi ndani ya timu hizo mbili ambazo zinatarajiwa kukutana Novemba 7, mwaka huu.
Onyango wa Simba ameshuhudia Aishi Manula akiokota kambani mabao matatu kwenye viwanja vya mikoani ambao alianza kushuhudia kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Sokoine wakati Simba ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Ihefu.
Kabla hajapoa, Onyango alishuhudia tena Manula akiokota mpira wa pili kwenye nyavu Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar.
Aliweka lango salama kwenye mchezo dhidi ya Biashara United wakati Simba ikishinda mabao 4-0 Uwanja wa Mkapa na mchezo wa Gwambina wakati Simba ikishinda mabao 3-0.
Uwanja wa Jamhuri, Dodoma akiwa kazini Onyango aliweka lango salama wakati Simba ikishinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania.
Mambo yalikuwa magumu Uwanja wa Nelson Mandela ambapo alimshuhudia Manula akiokota mpira wake wa tatu wakati wakichapwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.Pia ugumu ulizidi Uwanja wa Uhuru alipomshuhudia Beno Kakolanya akiokota mpira wake wa kwanza nyavuni na kufanya Simba ifungwa mabao manne ndani ya ligi.
Mwamnyeto amemshuhudia Faroukh Shikhalo akiokota wavuni bao moja ilikuwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya Tanzania Prisons.
Mechi nyingine ilikuwa ni mbele ya Kagera Sugar 0-1 Yanga, Mtibwa Sugar0-1 Yanga, Yanga 1-0 Mbeya City, Yanga 3-0 Coastal Union, Yanga 1- 0 Polisi Tanzania. Pia alimuona Metacha Mnata akiokota wavuni bao 1 wakati timu yake ikishinda mabao 2-1 dhidi ya KMC Uwanja wa CCM Kirumba.
Onyango akiwa ametumia dakika 630 ameshuhudia Manula akiokota langoni mabao matatu,na Kakolanya bao moja ana wastani wa kuruhusu hatari kila baada ya dakika 157 huku Mwamnyeto akiwa ametumia dakika 630 mabao mawili ameshuhudia timu yake ikifungwa.
We mwandishi huna jipya.
ReplyDeleteHapo unalazimisha stori tu. Ovyooo...
ReplyDeleteNi tangu lin onyango amekuw raia wa Uganda wee mwandishi
ReplyDeleteWaandishi acheni kukurupuka chukua muda kuediti kazi yako ni maisha yako vipi lakini sisi watanzania mbona tunakosa umakini katika mambo muhimu
ReplyDeleteHawa tunwaita vilaza kila uchwao, wamepata taaluma zao kwa kuibiaibia tu, sasa ndio madhara yake.
ReplyDeletehawana uwezo wa kupata habar sashihi