July 11, 2016


Shabiki wa Azam FC, Neema Mosha, jana Jumapili alijishindia jezi ya Yanga iliyosainiwa na wachezaji wote wa Yanga katika bahati nasibu iliyoendeshwa na Kampuni ya American Supermarket ambayo ni kampuni tanzu ya Quality Group.

Shindano hilo lilifanyika katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Quality Center jijini Dar ambapo Neema alikabidhiwa jezi hiyo na mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu huku akishuhudiwa na wachezaji wengine wa timu hiyo.

BABA DIDA (KUSHOTO)
Akizungumza baada ya kukabidhiwa jezi hiyo, Neema alisema: “Nimefurahi sana kupata zawadi hii, sitoigawa, nitakuwa naivaa lakini nitaendelea kuwa shabiki wa Azam FC kwani ninaipenda sana timu hiyo,” alisema.

Washindi wengine waliojinyakulia zawadi katika bahati nasibu hiyo ni Alex Munishi ambaye ni baba mdogo wa kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ ambaye alijishindia mpira. Hata hivyo mpira huo alimkabidhi Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ampelekee Dida.

Mshindi mwingine ni Ruteni, R G Mirambo ambaye alijishindia zawadi ya pikipiki.


Wachezaji wengine waliokuwepo kwenye ‘hafla’ hiyo ni Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV