Wakati Ligi Kuu Bara msimu wa 2015-16 inatarajia kuanza Agosti 20, mechi ya watani wa jadi, Yanga dhidi ya Simba itapigwa Oktoba Mosi.
Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga atakuwa mwenyeji wa Simba.
Timu hizo kongwe zitakutana baada ya kuwa zimecheza mechi sita tu kwa kuwa mechi hiyo ni mzunguko wa saba.
Maana yake, watani hao watakuwa ndiyo wamepasha moto kabla ya kukutana.
Mechi ya marudiano itakuwa ni Februari 5 ambayo itakuwa Jumapili na Simba watakuwa wenyeji.
Wakati zinakutana, Simba itakuwa na kumbukumbu ya kufungwa mechi zote mbili za msimu wa 2015-16. Kila mechi ilifungwa kwa mabao 2-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment