July 17, 2016


Ile sinema ya mshambuliaji Laudit Mavugo wa Vital’O kuwa anatarajia kutua Simba, imechukua sura mpya.

Taarifa zinasema, sasa yuko nchini Ufaransa kwa ajili ya kufanya majaribio katika klabu ya Tours FC ya nchini humo.

Rais wa Vital’O, Benjamin Bikorimana ambaye ni kama baba wa Mavugo, ameuthibitishia mmoja wa mtandao wa Burundi, kwamba yuko Ufaransa.

“Ndiyo yuko Ufaransa kwa ajili ya majaribio, tutawaeleza wakati mwingine,” alisema.


Taarifa zinaeleza, majaribio hayo ni ya wiki mbili, jambo ambalo linaonyesha kwamba hatajiunga tena na Simba na kama ni kweli, basi haiwezi kuwa hivi karibuni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV