RATIBA ILIYOZAGAA MTANDAONI |
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linaonekana kuhaha kuzuia ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara, iliyovuja.
Ratiba hiyo ya msimu wa 2016-17 inaonekana kuzagaa kwa kasi mitandaoni hali inayoonyesha kuwa imevuja.
Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amesema hakuna ratiba ambayo imetoka na hiyo haiwezi kuwa sahihi.
“Hakuna ratiba official, haiwezi kutoka kienyeji hivyo. Baada ya kuwa imetoka basi TFF itatangaza rasmi,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment