July 20, 2016


Klabu ya Stand Misuna imepoteza ushindi kwa mechi zote ambazo imemchezesha mchezaji Brown Chalamila kwa jina la Costa Bryan Bosco, kwa mujibu wa Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kadhalika kamati hiyo imepigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kila mechi ambayo wachezaji Brown Chalamila akitumia jina la Costa Bryan Bosco na Adolf Anthon akitumia jina la Fred John Lazaro wamecheza katika mashindano ya ligi ya mabingwa wa mkoa RCL kituo cha Morogoro 2015/2016.

Pia, kamati hiyo imeamua kwamba Seif Juma Maulid ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Stand Misuna FC kupelekwa Kamati ya Nidhamu kwa tuhuma za kughushi na kukamilisha zoezi la usajili kwa udanganyifu.

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefikia uamuzi huo kwa mujibu wa Kanuni ya 53, na kanuni ya 48 (3), 48 (4), 9(21), 36 (6) na kanuni ya 39 (1) adhabu kwa klabu katika kikao kilichoketi Julai 14, 2016 kujadilina, kupitia, malalamiko na taarifa za waamuzi na Kamisaa za mashindano ya RCL, Kituo cha Morogoro.

Kupitia malalamiko na vielelezo mbalimbali Kamati imebaini kwamba Misuna iliwasajili na kuwachezesha wachezaji Brown Chalamila akitumiaji na la Costa Bryan Bosco (3) na Adolf Anthony akitumia jina la Fred John Lazaro (13).


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV