July 20, 2016Real Madrid imeamua kuachana na kiungo Paul Pogba, imefahamika.

Pogba ni Mfaransa anayekipiga Juventus na amekuwa gumzo kwamba atatua Real Madrid au Manchester United. Taarifa zinaeleza, tayari wakala wake Mino Raiola raia wa Italia ameishaelezwa kuhusiana na uamuzi huo wa Madrid.

Lakini bench la ufundi la Madrid linaloongozwa na Zinedine Zidane linaonekana kuwa na furaha katakana na kikosi ilichonacho.

Maana yake, Manchester United pekee ndiyo itaendelea kupambana kwa ofa lie ya zaidi ya pauni million 100.

Kauli hiyo ya Madrid itachukuliwa kwa njia mbili, moja ni wanaweza kusema hivyo ili kupunguza bei ya kiungo huyo aliyeifikisha Ufaransa fainali ya Euro.


Au wanafanya hivyo, kweli wameamua kuachana naye kwa kuwa Madrid hawakuwa na tatizo la kiungo tokea msimu uliopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV