July 23, 2016

JUMA ABDUL, LEO ALFAJIRI WAKATI AKIONDOKA NA YANGA KWENDA ACCRA, GHANA

Beki wa kulia wa Yanga, Juma Abdul amesema ana imani kikosi chao kitapambana na kuishinda Medeama katikati kwa wiki ijayo jijini Accra.

Lakini akasisitiza, kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa msimu uliopita, kumempa nguvu ya kupambana zaidi.

“Najisikia nina nguvu zaidi, nitapambana zaidi kwa kuwa tuzo inaonyesha kuwa ninatakiwa kupambana zaidi ya hapa,” alisema.


“Kama timu ninaamini tutapambana, mechi itakuwa ngumu zaidi kwa kuwa tunacheza ugenini lakini tutafanya vizuri kwa pamoja,” alisema Juma Abdul wakati Yanga inaondoka kuifuata Medeama katika mechi ya Kombe la Shirikisho, leo alfajiri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV