July 11, 2016


Mashabiki wa Yanga, juzi walipagawa na staili ya kupiga kontroo ya beki wa kushoto wa timu hiyo, Oscar Joshua, ambaye ilikuwa ikielezwa na wengi siyo mtaalamu katika sekta hiyo.

Katika mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veterani, Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm aliwagawa wachezaji wake mafungu mawili na kuwataka kufunga mabao baada ya kuwa wamepiga mpira danadana kuanzia nje ya eneo la 18.

Wengi wakaanza kwa kupiga danadana kwa miguu yote huku mashabiki wengi waliokuwa nje ya uwanja huo wakisubiri zamu ya Joshua ambaye waliamini huwa hawezi.

Ilipofika zamu ya beki huyo alianza kwa kupiga kontroo akitumia goti hali ambayo iliwafanya mashabiki kushangilia, katika raundi ya pili,  Joshua alitumia kichwa kufika kwenye 18 kisha kupiga shuti na raundi ya tatu akatumia mguu wa kulia wakati yeye ni mtumiaji wa mguu wa kushoto ambapo pia alifika eneo la 18 na kupiga shuti lililodakwa na Kipa Benno Kakolanya.


Hali hiyo iliibua shangwe kubwa na kusababisha baadhi ya wachezaji wengine  wa Yanga nao kucheka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV