August 20, 2016

Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt amekamilisha ubabe wake wa kuchukua medali tatu ikiwa ni mara ya tatu kufanyua hivyo kwenye michezo ya Olimpiki.






     Bolt amefanya hivyo baada ya kukamilisha kupata medali ya dhahabu katika Olimpiki ambayo inaendelea nchini Brazil kwa kuchukua medali ya dhahabu katika mbio za mita 400 akiwa na wenzake wengine wane, ambapo walikuwa wakipokezana vijiti.
 
Bolt ambaye kabla ya hapo alikuwa na medali ya dhahabu katika mita 100 na mita 200 aliwaongoza wenzake kushinda kwa kukimbia kwa sekunde 37.27 wakifuatiwa na Wajapani waliokimbia kwa sekunde 37.60 huku Wacanada wakishika nafasi ya tatu kwa sekunde 37.64.

Waingereza waliokuwa wakijipa matumaini ya kufanya vizuri walishika nafasi ya tano kwa kukimbia sekunde 37.98.


Waingereza

Waingereza



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic