August 20, 2016

Mpira umemalizika: Full time, SIMBA 3-1 NDANDA FC
 
Dakika 90 + 2: Muda wowote mchezo utamalizika.


Dakika ya 90: Mwamuzi anaongeza dakika mbili za nyongeza.
 
Dakika ya 88: Mavugo anakosa nafasi ya wazi, anampiga chenga kipa Chove kutoka pembeni kisha anapiga shuti ambalo linatoka nje.
 
Dakika ya 86: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Kichuya anaingia Ibrahim.
 

Dakika ya 81: Simba wanaonekana kuamka, bao la Kichuya bado linaonekana kujadiliwa na watu wengi uwanjani hapa kutokana na jinsi alivyopiga shuti kali.

Dakika ya 74: Simba wanapata bao la tatu mfungaji akiwa ni Kichuya baada ya kuunganisha mpira wa kona uliopanguliwa kisha akapiga shuti kali.

Dakika ya 73: Sima wanapata bao la pili kupitia kwa Blagnoun ambaye anafunga kwa kichwa akiunganisha mpira uliotoka pembeni.
 
Dakika ya 70: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Mnyate anaingia Mwinyi Kazimoto.

Dakika ya 70: Ndanda wanapiga pasi na kuelewana.
 
Dakika ya 67: Mchezo bado mgumu kwa timu ote, Ndanda wanaonekana kuanza kuelewana tofauti na kipindi cha kwanza.

Dakika ya 62: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Ibrahim Ajib anaingia Blagnon raia wa Ivory Coast. 

Dakika ya 50: Simba wanafanya mashambulizi makali.

Dakika ya 46: Kipindi cha pili kimeanza.
 
Kipindi cha kwanza kimekamilika Simba 1-1 Ndanda FC
 
Dakika ya 45: Zimeongezwa dakika mbili.

Dakika ya 43: Mchezo umebalansi, timu zote zinaonekana kuwa makini kujilinda.
 
Dakika ya 38: Bao la kusawzisha linawapa nguvu Ndanda ambao sasa wanaoenekana kuamka.

Dakika ya 36: Ndanda wanasawazisha bao kupitia kwa Omary Mponda ambaye anafunga bao zuri kwa kichwa, akiunganisha mpira wa faulo uliopigwa na Kiggy Makassy.
 
Dakika ya 31: Mavugo anakosa nafasi ya wazi baada ya mpira aliopuga kwa kicha kutoka nje kidogo ya goli. Ndanda wanashindwa kumzui Mavugo ambaye anakuwa ni msumbufu kwao muda mwingi.
 
Dakika ya 25: Simba bado wanatawala mchezo na wamemiliki kwa asilimia kubwa huku wakipata shangwe nyingi kutoka kwa mashabiki wao.

Dakika ya 19: Mavugo anaipatia Simba bao baada ya kuunganisha mpira wa faulo. Simba inaongoza bao 1-0. Faulo ilipigwa na Zimbwe JR ambaye zamani alikuwa akijulikana kwa jina la Tshabalala.
 
Dakika ya 17: Mchezo unaendelea, Ibrahim Ajib wa Simba anapata kadi ya njano kwa kuonekana kama amejiangusha ndani ya eneo la hatari

 Dakika ya 16: Kipa wa Ndanda, Jackson Chove ameumia goti na mchezo umesimama anatibiwa.
 
Dakika ya 13: Ndanda wanaanza kuamka kidogo kidogo, Simba wanatoa presha kwa lengo la kutaka kupata bao la mapema lakini bado ngome ni ngumu.

Dakika ya 8: Simba bado wanatawala mchezo huku Ndanda wakiongozwa na mshambuliaji wao, Shija Mkina wakipambana kurejesha majibu.


Dakika ya 5: Simba bado wamemiliki mpira na Mavugo tena anakosa nafasi ya wazi kwa kupiga shuti kali linalopanguliwa na kipa. 

Dakika ya 1: Mavugo anapiga shuti kali ambalo linapanguliwa na kipa wa Ndanda lakini wachezaji wa Simba wanakuwa mbali kumalizia.
 
Mchezo umeanza, Simba wanafanya shambulizi kali.
 
Muda wowote mchezo utaanza, kaa tayari kupata kila kitu kutoka hapa Uwanja wa Taifa.

Timu ndiyo zinaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza mchezo.

Kikosi cha Simba kitakachoanza katika mechi ya leo hiki hapa:

1. Vicent Angban
2. Malika Ndeule
3. Mohamed Zimbwe
4. Method Mwanjale
5. Juuko Murshid
6. Jonas Mkude
7. Shiza Kichuya
8. Mohammed Ibrahim
9. Laudit Mavugo
10. Ibrahim Ajib
11. Jamal Mnyate

Benchi:
Peter Manyika (GK)
Hamad Juma
Novaty Lufunga
Frederic Blagnon
Mussa Ndusha
Muzamir Yassin
Mwinyi Kazimoto
 
Msimu mpya wa 2016/17 unafunguliwa rasmi ambapo kutakuwa na mechi kadhaa katika mikoa tofauti, ambapo mtanange unaotazamwa na wengi ni ule wa Simba dhidi ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambayo inatarajiwa kuanza muda siyo mrefu kutoka sasa.
 

2 COMMENTS:

  1. Line up ya Simba Beki 2 alikuwa Hamad Juma sio Malika Ndeule

    ReplyDelete
  2. Line up ya Simba Beki 2 alikuwa Hamad Juma sio Malika Ndeule

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic