August 21, 2016

Staa wa Barcelona, Neymar, usiku wa kumkia leo ametimiza ndoto ya taifa lake la Braz,ila kutwaa ubingwa wa soka katika michezo ya Olimpiki baada ya mtihani huo kuwashindwa kaka zake wengi waliocheza katika taifa hilo miaka iliyopita.
 
Brazil imepata ubingwa huo kwa kuifunga Ujerumani kwa penalti 5-1 baada ya matokeo ya bao 1-1 katika dakika 90 kisha hata zilipoongezwa dakika 30 kuwa 120 bado matokeo yalikuwa 1-1. Neymar ndiye aliyekuwa wa kwanza kufungua ukurasa wa mabao kwa kufunga bao katika dakika ya 27 kwa njia ya faulo.

Ujerumani ilisawazisha bao hilo kupita kwa Max Meyer katika dakika ya 59.  

 
Neymar akishangilia kwa staili kama ya Usain Bolt


Usain Bolt naye alikuwepo kushuhudia Brazil ikifanya yake.
Baada ya hapo kilichofuata ni matuta ambapo Brazil ilipata penalti zote tano huku Ujerumani ikiondoka kichwa chini kwenye Uwanja wa MaracanĂ£ uliopo Rio de Janeiro baada ya mchezaji wao, Nils Petersen kukosa penalti ya mwisho.

Akizungumza baada ya mchezo huo Kocha wa Brazil, Rogerio Micale alisema: "Soka la Brazil halijafa, nchi mwenyeji wametaa ubingwa katika staili ya kipekee.


 


Ushindi huo ni kama kisasi kwa Brazil ambayo ilifungwa mabao 7-1 na Ujerumani katika Kombe la Dunia 2014.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV