August 19, 2016


Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali ameendelea kuwa kichwa cha habari kwenye vyombo vya habari na mitandao.

Safari hii ameibuka na kusema vijana wanaondeshwa na viroba wameshindwa kujitokeza nyumbani kwake kama walivyoahidi.

Akilimali, jana alipiga mkwara akisema anayetaka kutengana na familia yake kwa muda usiojulikana, avamie kwake.

“Wameshindwa, maana walisema nimekimbia lakini mimi nipo kwangu.

“Wanauendeshwa na viroba, wanachukulia kila kitu rahisi. Wangekuja sasa waone, mimi si mtu mgomvi lakini sifurahii kuona watu wanataka kunipa hofu kisa nimetoa maoni.

“Kitu kibaya zaidi mimi nimeomba radhi na kufuta kauli yangu, lakini bado wananisakama na kutaka kunifanya niishi kama mkimbizi, wangekuja waone,” alisisitiza.


Kumekuwa na taarifa kwamba kuna mashabiki wa Yanga wanataka kuvamia kwake kwa madai yeye amekuwa chanzo cha Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kusema atapumzika na kuachana na Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV