Kwa mara ya kwanza Azam Media Ltd wakishirikiana na TDE (The family of Toussaint Duches Entartainment) kutoka nchini Marekani wameungana na vipaji vya wasanii maarufu wa sanaa ya Uigizaji Tanzania wanakuletea “Souper Soul Sunday” maonyesho makubwa ya mchezo wa kuigiza ambayo imechukua sehemu kubwa ya kumbi za maonyesho na kujizolea umaarufu mkubwa Marekani.
Akizindua rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media Ltd, Tido Mhando alisema kuwa huu ni msimu wetu mpya wa Burudani na tumejipanga kila sekta kuja kivingine na hata sanaa ya maigizo ni moja kati ya vipengele muhimu sana kwetu na hata tukaweka channeli ya Sinema Zetu inayorusha Filamu za Tanzania ikiwa njia ya kuburudisha na kukuza sanaa yetu ya maigizo.
“Tumeungana na TDE kwa kuwa tunataka kuwa wa kwanza kuwaletea Souper Soul Sunday ambayo familia huungana kila Jumapili hiyo kufurahi, kula, kunywa kuburudika na muziki na kumalizia na Igizo hilo maalum lililoandaliwa siku hiyo ambapo kwa sisi litakuwa ni Mrs Lucy Goes to Africa” Alisema Tido.
Nae Muigizaji/Mtunzi na Mkurugenzi mtendaji wa TDE Lady Toussaint Duchess Campbell (Lady T) alisema kuwa Soul Sunday itakuja na Igizo maalum la “Mrs Lucy Goes to Africa” kwa mtindo wa Broadway, ikishirikisha wasanii maarufu kutoka Tanzania wakiwemo “Natasha” na “Monalisa” itafanyika hapa Dar es Salaam tarehe 14/8/2016 kuanzia saa 9:00 Alasiri katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa yaliyopo Barabara ya Shaaban Robert Posta kiingilio ni shilingi 80,000.
Souper Soul Sunday itasindikizwa na burudani ya muziki wa Jazz na chakula maalum kilichojizolea umaarufu nchini Marekani aina ya “Gumbo”.
Lady Toussaint Duchess Campbell (Lady T) aliongeza kuwa Souper Soul Sunday inaleta msukumo wake wa kwanza, kimuziki kisanaa ya jukwaani naigizo la “Mrs Lucy Goes to Africa” ni la kipekee na la aina ya kuchekesha ambayo italeta burudani kwa familia kwa kiwango kikubwa.
“Ukumbi wa michezo wa Afrika na Marekani wameunganisha maonyesho yao ya kipekee kuleta kitu kipya na cha kusisimua Dar Es Salaam, ni ushirikiano ambao hauta sahaulika” alisema Duchess.
Mrs. Lucy Goes to Afrika huu sio mchezo tu Super Soul Sunday imeanza na ladha ya Marekani Kusini katika muundo wa vyakula vya kuridhisha bakuli la ''Gumbo''. Pamoja na maongezi mazuri na muziki laini. Chakula kitafatiwa na ''Mrs. Lucy Goes to Afrika'', ambayo itakufanya ucheke ne kulia lakini itakuacha na meseji nzuri ya matumaini na faraja na zaidi ya hayo itakufanya utake kuiona tena na tena.
''Kuna zaidi katika kazi kwa TDE na UPL Production na AzamTV alisema Tito Mhando , kinacholetwa na UPL ni sawa na ambacho tumekuwa na ndoto nacho...sasa tufanye ndoto iwe kweli na hichi ndicho Dar es Salaam inahitaji anasema.
Tiketi zinapatikana kwa pesa kwa kupiga namba 0765 593288. Pia zina weza kunuliwa AzamTV, Clouds Mikocheni, Woodbery Cafe, Tabasamu PR Mbezi Beach, Epidor Masaki, Samaki Samaki na Mr. price Mlimani City na Makumbusho ya Kihistoria.
Welcome to CommHubb – you now own a piece of it!Just click the link below!
ReplyDeletehttp://www.commhubb.com/affiliate.php?ref=205643