August 15, 2016


Licha ya Kocha Arsene Wenger kudai kuwa kipigo cha mabao 4-3 ambacho timu yake ilikipata jana Jumapili kutoka kwa Liverpool, kimetokana na wachezaji wake kuwa majeruhi na wengine kutokuwa fiti, mshambuliaji mkongwe wa zamani wa timu hiyo, Thierry Henry amekosoa mfumo unaotumika ndani ya Arsenal.

Henry amesema kuwa anashindwa kuelewa kwa nini timu yake hiyo inashindwa kuweka fedha sokoni kisha ikashindana na timu nyingine kubwa katika kuwania wachezaji wenye uwezo mkubwa licha ya kutajwa kuwa ni moja ya klabu tajiri.

“Kitu ninachoshindw akukielewa ni kuwa Arsenal inatajwa kuwa klabu tajiri lakini inashindwa kushindana sokoni kuwania wachezaji," alisema Henry alipokuwa akizungumzia juu ya mwenendo wa Arsenal, kisha akaongeza kwa kusema: 


 "Unadhani wachezaji wakubwa watavutiwa kuichezea Arsenal? Unadhani klabu ina mifumo ya kuwavuta? hayo ni maswali unayotakiwa kujiuliza.”

Thierry Henry ametamka hayo siku chache tangu alipoondoka klabuni hapo na kuachana na mafunzo ya ukocha aliyokuwa akiendelea nayo klabuni hapo baada ya Wenger kumtaka achague moja kati ya kuendelea kuwa klabuni hapo kufundisha au kuwa mchambuzi kwenye uninga.

Kauli hiyo ni mwendelezo wa lawama nyingi ambazo Wenger amekuwa akitupiwa akionekana ni mzito kufanya maamuzi ya kusajili wachezaji wakubwa ambapo Henry amesema anaamini Arsenal bado inahitaji straika mmoja na beki wa kati.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV