August 22, 2016

Licha ya kumalizika kwa michuano ya Olimpiki, jana, mshambuliaji wa Barcelona, Neymar anatarajiwa kukosa mechi ya timu yake hiyo wikiendi hii dhidi ya Athletic Bilbao katika La Liga kutokana na kupewa muda wa ziada wa kupumzika. 





Imeelezwa kuwa Neymar hatarejea Hispania ndani ya siku chache zijazo ili aupumzishe mwili baada ya kuiwezesha Brazil kutwaa ubingwa wa Olimpiki katika soka kwa kuifunga Ujerumani kwa penalti 5-4.

Taarifa kutoka Hispania zimeeleza kuwa Kocha wa Barcelona, Luis Enrique amempa muda wa kupumzika mchezaji huyo hadi Septemba, mwaka huu.

 

Wakati huohuo, mara baada ya kutwaa ubingwa huo wa Olimpiki, Neymar ameamua kujiweka pembeni katika suala la kuwa nahodha wa Brazil.

“Lilikuwa jambo la faraja sana uwa nahodhalakini kuanzia leo nimejiodoa na nitatuma ujumbe kwa benchi la ufundi na wenzangu ili achaguliwe nahodha mwingi," alisema Neymar ambaye imeeleza sababu za kufanya hivyo ni kupunguza presha aliyokuwa kiipata kutokana na yeye kubeba majukumu hayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic