August 22, 2016

Wachina waliokuwa wakiukarabati Uwanja wa Uhuru wa jijini Dar, leo Jumatatu wameukabidhi mikononi mwa Serikali ya Tanzania baada ya kumalizika kwa marekebisho yake yaliyoanza mwaka 2013.

Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) ya nchini China ambayo ilikuwa ikisimamia marekebisho ya uwanja huo chini ya meneja wake mkuu, Cheng Longhai, walimkabidhi Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye katika hafla fupi iliyofanyika uwanja hapo, mapema hii leo.
 

Akizungumza baada ya kukabidhiwa uwanja huo maarufu kwa jina la Shamba la Bibi, Nape alisema: “Ni jambo la busara kwa kila atakayeutumia uwanja huu kuwa mlinzi kwa mwenzake ili kulinda miundombinu yake ili udumu kwa miaka mingi zaidi kwani hii ni hazina yetu sote.”

Wakati huohuo, mbunifu wa michoro ya uwanja huo, Aloyse Peter Mushi, alisema: “Uwanja huu unaingiza watu waliokaa elfu 23, lakini wakikaa kwa kubanana wanafika elfu 25, tulianza marekebisho haya mwaka 2013, na tunashukuru leo hii umekamilika na serikali kukabidhiwa.”


  
Muonekano wa Uwanja wa Uhuru

Muonekano wa Uwanja wa Uhuru

Mara baada ya makabidhiano

Mwakilishi wa Kampuni ya Beijing Constructionakifafanua jambo wakati wa makabidhiano hayo.



Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipata maelekezo kutoka kwa katibu mkuu wa wizara yake, Profesa Elisante Ole Gabriel.

Waziri Nape akizungumza.

Baada ya uwanja huo kukamilika na kukabidhiwa mikononi mwa serikali, sasa utaanza kutumika kwa mechi mbalimbali ikiwemo za Ligi Kuu Bara msimu huu. Mara ya mwisho kwa uwanja huo kutumika kwa mechi kama hizo ilikuwa ni mwaka 2010.

1 COMMENTS:

  1. Karne hii kukaa kwenye sementi?
    Hivyo viti ni lile jukwaa kuu la zamani. Wachina wameongeza mengine lakini hakuna viti. Ni mwendo wa kukaa kwenye sementi. What a shame!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic