August 21, 2016

Mara baada ya kuiongoza timu yake kupata ushindi katika mechi ya pili mfululizo kwenye Ligi Kuu ya England ‘Premier League’, straika wa Chelsea, Diego Costa ametupia mtandao picha ambayo imewachanganya watu wengi kutokana na jinsi ilivyo.

Picha hiyo inamuonyesha Costa akiwa na kaka yake, Jair kwenye ukurasa wake wa Instagram lakini kutokana na wawili hao kufanana wapo ambao wameshindwa kumtambua Costa ni yupo hasa kwa kuwa Diego mwenyewe alichoamua ni kunyoa ndevu mara baada ya mchezo wa jana.   Picha hiyo imewafanya baadhi kuamini kuwa yawezekana ni mapacha lakini baada ya kufuatilia maelekezo wanagundua kuwa wawili hao ni mtu na mdogo wake na siyo mapacha.

Costa alikuwa na ndevu nyingi kama ilivyo kwa kaka yake huyo lakini mara baada ya mchezo dhidi ya Watford, aliamua kwenda kunyoa ndevu, sasa baadaye aakapiga picha na kaka yake huyo hali ambayo imesababisha wengi kupata kifra kuwa yule mwenye ndevu ndiye Costa kitu ambacho siyo sahihi.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV