Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameongoza mamia ya wananchi kuuaga mwili wa mwanamuziki mkongwe wa taarabu Shakila Said Hamis maarufu kwa jina la ‘Bi Shakila’, leo jijini Dar.
Mwili wa Bi Shakila Said umehifadhiwa katika nyumba yake ya milele maeneo ya nyumbani kwake Mbagala Charambe jijini Dar.
APUMZIKE KWA AMANI, AMINA!
PICHA: MICHUZI-MATUKIO
Bi Shakila enzi za uhai wake. |
Mwili wa Bi Shakila Said umehifadhiwa katika nyumba yake ya milele maeneo ya nyumbani kwake Mbagala Charambe jijini Dar.
Rais
Mstaafu awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete (wa tatu kulia) akijalidiliana
jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
(pili kushoto).
|
Makamu
wa Rais Mh, Samia Suluhu akijadiliana jambo na mmoja wa waombolezaji
nyumbani kwa marehemu, kabla ya maziko kufanyika. Bi Shakila, amefariki
ghafla nyumbani kwake, huko Mbagala Charambe.
|
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akizungumza na waombolezaji.
|
Katibu MKuu wa Shirikisho la Wanamuziki Tanzania, John Kitime akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said, nyumbani kwa marehemu Mbagala Charambe jijini Dar.
|
Makamu
wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiweka saini kitabu cha maombolezo
cha Bi Shakila Mbagala Charambe jijini Dar, kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye.
|
Baadhi
ya wanamuziki wakongwe na Bongo Fleva wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kushiriki mazishi ya Bi Shakila huko nyumbani kwake Mbagala
Charambe jijini Dar.
|
APUMZIKE KWA AMANI, AMINA!
PICHA: MICHUZI-MATUKIO
0 COMMENTS:
Post a Comment