August 21, 2016

Mwanariadha wa Tanzania, Alphonce Felix Simbu ameshika nafasi ya tano katika mbio ndefu za wanaume kwenye michezo ya Olimpiki.

Tanzania ambayo haijawa na matokeo mazuri wala kupata medali katika michezo hiyo ambayo inafungwa leo nchini Brazil, angalau inaweza kupata tabasamu kutokan na matokeo hayo.
Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu ambayo asilimia kubwa ilikuwa ikifanyika jijini Rio de Janeiro ilifunguliwa rasmi Agosti 5, mwaka huu na kushuhudia Marekani ikitawlaa kwa kupata medali nyingi.

Mataifa yaliyoongoza kwa medali katika michezo hiyo ni

                        Dhahabu fedha shaba jumla
1. Marekani       43     37     37     117
2. Uingereza     27     22     17     66
3. China            26     18     24     68
4. Russia          17     17     18     52
5. Ujerumani     17     10     14     41
6. Japan           12     8       21     41
7.  Ufaransa       9     17     14     40

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV