August 2, 2016


Bilionea Mohammed Dewji ameanza kazi katika klabu ya Simba baada ya kutoa Sh milioni 100 kusaidia usajili.


Mo ametoa fedha hizo leo na kuzikabidhi kwa Rais wa Simba, Evans Aveva.

Mo alikubali kuisaidia Simba katika usajili wakati mchakato wa kwenda kwenye mabadiliko na kuwa kampuni ukiendelea.

Tayari bilionea huyo kijana ametangaza kumwaga fedha Sh bilioni 20 ili kupata hisa asilimia 51 ya umiliki wa klabu hiyo na wanachama wameridhia katika mkutano wa wanachama uliofanyika juzi Jumapili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV