August 21, 2016

Baada ya kuichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, timu ya Ruvu Shooting imeanza tambo ya kuwaitafanya vizuri huku ikiendeleza ule msemo wake kuwa imedhamiria kuwa Leicester City ya Bongo.
 

Tangu ipande daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza, Ruvu imekua aikijinasibu kuwa imejipanga vizuri na inataka kufanya kweli kwa kutwaa ubingwa wa msimu huu katika Ligi Kuu Bara kama ambavyo Leicester City ilivyofanya msimu uliopita katika Premier League licha ya kuwa ilikuwa haipewi nafasi.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa walijua kuwa wanaenda Manungu kuchukua pointi zao tatu na ndiyo maana hawakuwa na presha, huku akisisitiza imani yao hiyo ya kufanya maajabu ya kutwaa ubingwa.


Masau Bwire akiwa kibaruani kwake nje ya soka.

Kauli hiyo hiyo inaweza isiwe nzuri kwa Simba na Yanga pamoja na Azam FCF ambazo ndizo timu zinazotajwa kuwa na nguvu ya kutwaa ubingwa kutokana na usajili uliofanyika kwenye timu hizo.

Bwire ambaye kitaaluma ni mwalimu amesema kuwa baada ya usindi huo sasa wanaelekeza nguvu zao kwa Tanzania Prisons ya Mbeya ambao ndiyo wapinzani wao katika mchezo unaofuata mnamo Agosti 20, mwaka huu.
 

Leicester City
"Moto umeshawaka na hakuna wa kuuzima, tumeanza na Mtibwa, sasa tunawataka Prisons wakae mkao wa kufungwa," alisema Bwire.

Matokeo ya jumla ya mechi za ufunguzi wa Ligi Kuu Bara 2016/17 zilizochezwa jana ni haya hapa:
Simba        3-1    Ndanda FC   
Stand         1-1    Mbao FC   
Mtibwa         0-1    Ruvu Shooting
Azam FC        1-1    Lyon   
Majimaji FC    0-1    Prisons
   

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV