NIKIWA CAMP NOU DAKIKA CHACHE KABLA YA MECHI YA BARCELONA VS REAL BETIS KUANZA |
Nilikuwa uwanjani wakati Barcelona ikianza La Liga na kuitwanga Real Betis kwa mabao 6-2.
Luis Suarez akatupia Hat Trick na Lionel Messi akafunga mabao mawili hivyo kuwafanya mabingwa hao kuanza ligi kwa kishindo.
Kwa mashabiki wa Barcelona ni jambo jema lakini mimi niliendelea kujifunza mengi kuanzia nje ya uwanja hadi ndani.
Utamaduni wa watu wa Barcelona unaweza kuwa tofauti na wale wa Madrid lakini asilimia 90 ni wale wanaotaka kuona kila kitu kinakwenda kwa amani.
Idadi kubwa ya wazee wenye umri kuanzia miaka 70 kwenda juu walikuwa uwanjani kwa wingi, jambo ambalo linaonyesha ni tofauti.
Lakini idadi ya watoto na kinadada ni kubwa sana, jambo ambalo linaongeza burudani zaidi uwanjani.
Lakini wafanyakazi wa eneo la uwanja ni wacheshi na wanaotaka kuona kila mtu anafurahia kilichompleka.
Maana ya kwenda uwanjani inatimia na kuondoa hisia soka ni yale mabao tu, badala yake hata watu wanavyokutana na kufurahi pamoja kuanzia nje ya uwanja hadi ndani.
0 COMMENTS:
Post a Comment