August 18, 2016Mshambuliaji Mzimbabwe wa Yanga, Donald Ngoma ameanza na mabao mawili katika mechi ya kwanza tu ya upashaji misuli kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi.

Katika mechi hiyo ya Ngao ya Jamii, jana. Ngoma alifunga mabao mawili ya Yanga ambayo mwisho, mabeki walizembea na Azam FC wakasawazisha na kuwa 2-2.

Lakini kwa uchezaji, Ngoma alionekana ametulia sana na ana uwezo wa kufunga zaidi kwa kuwa msimu ujao, atakuwa ameizoea zaidi ligi.

Msimu uliopita alimaliza na mabao 17, lakini ndiyo alikuwa mgeni. Kuna uwezekano mkubwa, akafanya vizuri zaidi kama kikosi cha Yanga kitaendelea kucheza kwa kasi na mpira wa kushambulia kama ambavyo imekuwa kwa misimu miwili mfululizo.

Ngoma ana nafasi nzuri ya kufunga zaidi kwa kuwa si mwoga, pia ni mtu mwenye kiu ya mabao. Lakini mabeki wameanza kuingiwa hofu dhidi yake, jambo ambalo litamsaidia zaidi kujiamini.


Kingine kinachomfanya azidi kuwa zaidi ni kuweza kuhimili kupunguza jazba ambazo zilikuwa zikimtoa “nje ya reli”. Kitu ambacho mabeki wengi wamekuwa wakikitumia.

1 COMMENTS:

  1. Mbona live stream ya Azam sports Hd imekata tatizo nn kaka saleh

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV