August 20, 2016

Ikicheza mbele ya mashabiki zaidi ya 75,000 waliojitokeza kwenye Uwanja wa Old Trafford, Manchester United imeendelea kuwa na mwanzo mzuri kwenye Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ baada ya kuifunga Southampton mabao 2-0.

 
Mchezo huo ambao ulichezwa usiku wa kuamkia leo, ulishuhudiwa pia na mamilioni ya watu duniani kupitia runinga ambapo mabao ya straika mkongwe wa timu hiyo, Zlatan Ibrahimovic yalitosha kuipa ushindi huo na hivyo kufikisha pointi sita katika mechi mbili ilizocheza mpaka sasa katika ligi hiyo.







 
Kwa mabao hayo ya Ibrahimovicm yanakuwa ni mabao matatu katika mechi mbili za ligi hiyo kwake, ikiwa ni mwendelezo wa kufanya vizuri katika ligi kuu za ncho tofauti alizocheza.

Wayne Rooney alipiga krosi murua iliyounganishwa kwa kichwa na Zlatan ambaye aliandika bao la kwanza katika dakika ya 36, licha ya wapinzani wao hao kuanza vizuri kwa kuwabana United katika dakika za mwanzo.  





United ambayo pia ilikuwa ikimtumia mchezaji wake, Paul Pogba kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Juventus ya Italia, ilionekana kujiamini tofauti na msimu uliopita ilipokuwa chini ya Kocha Louis van Gaal.

Zlatan aliongeza bao la pili kwa njia ya penalti katika dakika ya 52 baada ya beki wa kushoto wa timu hiyo, Luke Shaw kuchezewa vibaya ndani ya eneo la hatari.

Mchezo huo ulikuwa na upinzani mkali hasa kipindi cha kwanza ambapo Southampton ilifanya mashambulizi kadhaa lakini ikashindwa kutumia vizuri nafasi ilizopata.

Katika mchezo huo Pogba alionyesha uwezo mzuri licha ya kuanza kwa kasi ndogo ambapo muda mwingi alionekana kujiamini na kuichezesha timu hasa katika kupandisha mashambulizi huku kocha wake, Jose Mourinho akiwa amesimama muda wote akitoa maelekezo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic