August 19, 2016

Simba ipo katika harakati za kuujenga uwanja wake wa mazoezi uliopo Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam lakini sasa habari nzuri ni kuwa tayari ramani ya uwanja huo imeshazinduliwa na kuwavutia wengi.
 

Mbali na uwanja huo wa mazoezi, ramani iliyozinduliwa na kuonyeshwa na klabu hiyo imeonyesha jinsi ambavyo uwanja huo wa mazoezi na ule mwingine mkubwa utakavyokuwa.   Uwanja wa mazoezi Simba imesema kuwa itaujengea ukuta uwanja huo ili kuzunguka kwa ajili ya ulinzi, pia mbali ya uwanja mpya mkubwa lakini pia kutakuwa na hosteli jirani na vilipo viwanja hivyo vyote viwili.

Uongozi wa Simba chini ya rais Evans Aveva ulizindua ramani hiyo wakati ulipotembelea uwanja huo huku mchakato wa kuchangishana matofali ya kujengea uwanja huo ukianza.

Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini, Mzee Hamisi Kilomoni aliitambulisha ramani ya uwanja huo. Alianza kwa kufungua kitambaa kilichoficha ramani na kuionyesha kwa mashabiki wa timu hiyo waliofika kwenye uzinduzi huo.

Ramani hiyo ya uwanja, inaonyesha kuwepo uwanja mkubwa utakaotumika kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara na mashindano mengine.

Uwanja mkubwa utakaotumika kwa ajili ya mechi za mashindano, mbele yake wameandaa sehemu nzuri za maegesho ya magari ya mashabiki na viongozi.

2 COMMENTS:

  1. ile ramani ya wale waturuki waliowaletaga huko nyuma waliachana nayo?au watazitumia zote tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. unazungumzia zile raman 3 za manji akasema mchague moja?

      Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV