August 27, 2016


TUNAWAMBA RADHI WASOMAJI WETU KUTOKANA NA KUSHINDWA KUENDELEA KUWALETEA LIVE WASOMAJI WETU KUTOKANA NA MATATIZO YALIYOJITOKEZA KWENYE MTANDAO WETU.

Mechi kati ya Simba DHIDI ya RUVU JKT imeisha kwa sare ya bila bao.
Dk 35, Kichuya anaingia vizuri katika eneo la hatari akichambua lakini anakuwa mchoyo na mabeki JKT wanaokoa kwa urahisi kabisa
Dk 32, Kichuya anaingia vizuri na kupiga krosi maridadi kwa Mkude ambaye anapiga shuti nyanya
Dk 26, Simba wanagongeana, krosi nzuri ya Zimbwe Jr, lakini Mavugo anachelewa

SUB: Dk 24, JKT wanamtoa Michael Aidan anaingia James Msuva, huyu mdogo wa damu wa Simon Msuva wa Yanga
Dk 20, Kichuya anapiga shuti mpindo lakini kipa JKT anafanya kazi ya ziada na kuokoa, kona. Inachongwa na Zimbwe Jr lakini unaokolewa na kuwa wa kulusha
Dk 17 sasa, mashambulizi mawili tu ya JKT yanaonekana kuwa makali huku Simba wakipoteza kasi waliyoanza nayo na kupoteza pasi nyingi sana

Dk 16, Saada Kipanga anaingia vizuri Mwanjale anaokoa, mpira unamkuta Atupele Green naye anapiga shuti kidogo na Lufunga anauchukua kwa ulaini
Dk 15, Lufunga anafanya kazi nzuri kuokoa krosi ya JKT Ruvu na kuwa kona. Inachongwa na Salum Gilla, lakini Angban anadaka vizuri kabisa
Dk 14, krosi nzuri ya Mnyate, Mavuto na Blagnon wanajichanganya wenyewe
Dk 13, Mavugo anapata nafasi ya kupiga mpira uliokufa, lakini mpira unapaa juuu..
Dk 11, bado mpira unapigwa katikati ya uwanja zaidi huku JKT wakiendelea kubaki bila ya shuti hata moja langoni mwa Simba
Dk 7, hadi sasa, JKT hawajafanya hata shambulizi moja wala kuingia kwenye 18 ya lango la Simba ingawa katikati ya uwanja kunakuwa na ushindani mkali.

Dk 5, Simba wanafanya shambulizi jingine, lakini wanaonekana wanashindwa kumalizia vizuri kama ilivyokuwa kwa mashambulizi mengine mawili ya mwanzo.
Dk 3, Simba wanafanya shambulizi jingine safi, Mnyate anaingia vizuri, anapiga shuti lakini beki JKT anazuia vizuri na kuokoa
Dk 1, Mpira umeanza taratibu Simba wakianza kwa kasi zaidi na Shiza Kichuya anaingia kwa kasi na kupiga shuti kali, lakini hakulenga lango

2 COMMENTS:

  1. we vip mbn huendelei kutupa updates?

    ReplyDelete
  2. Enter your comment...Yawezekana kimewaka mnyama

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV