Kikosi cha Azam FC leo kitashuka dimbani kuvaana na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Chamazi uliopo nje kidogo mwa Jiji la Dar ikiwa ni moja ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Azam ilikwenda kuweka kambi ya wiki moja Visiwani Zanzibar lakini imerejea wikiendi iliyopita ambapo kocha anatumia muda huu kuwachunguza wachezaji wake anaowahitaji kuwasajili.
Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Idd amefunguka kwa kusema kuwa, kocha wa timu hiyo Mhispania Zeben Hernandez amehitaji mechi kadhaa kwa ajili ya kukipima kikosi chake ikiwa ni pamoja na kuangalia wachezaji atakaowasajili ambapo ataanza kucheza na JKT Ruvu kisha Ruvu Shooting.
“Jumatano tutacheza na JKT Ruvu kisha tunaendelea na mazungumzo ya kukutana na Ruvu Shooting tutakaocheza nao wikiendi hii mechi ambazo amezipendekeza kocha ili kuangalia wachezaji atakaowasajili.
“Kocha ameamua kutoa taarifa yake ya usajili ndani ya wiki hii ambapo atakabidhi majina ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa na uongozi kufanya uamuzi,” alisema Jaffar.
0 COMMENTS:
Post a Comment