August 3, 2016


Kama utani vile, straika mpya wa Simba, Ame Ali amepokelewa vizuri na mashabiki wa timu hiyo baada ya kujitokeza kwa wingi kumshuhudia kwa mara ya kwanza akiwa na jezi za wekundu hao wa Msimbazi.

Ame aliyejiunga na Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Azam FC, alianza mazoezi na kikosi hicho juzi Jumatatu asubuhi na jioni kucheza mechi yake ya kwanza ya kirafiki akiwa na jezi za Simba ambapo alionyesha kiwango kizuri.

Awali hakuna shabiki aliyekuwa akijua kama kuna ujio wa Ame, lakini baada ya kumuona uwanjani jioni kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Burkinafaso, wakaanza kuitana na dakika chache tu uwanja ukafurika mashabiki wakitaka kumshuhudia staa huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar.

Hata hivyo, mashabiki walisubiri mpaka kipindi cha kwanza kilimalizike ndiyo wamuone uwanjani, kwani alianzia benchi. Ame aliingia kipindi cha pili kilipotaka kuanza akichukua nafasi ya Ibrahim Ajib na kucheza kwa kujiamini kama vile alikuwepo na wenzake hao kwa siku nyingi huku mashabiki wakimshangilia kila aliponasa mpira.


1 COMMENTS:

  1. Welcome to CommHubb – you now own a piece of it!Just click the link below!
    http://www.commhubb.com/affiliate.php?ref=205643

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV