August 6, 2016Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameanza kuzungumza na wanachama wa klabu hiyo kwenye na kusema haungi mfumo wa hisa kwa kuwa ni klabu ya wanachama.

Mkutano huo wa dharura ulioitishwa na Manji unafanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.


Maneno hayo ya Manji, maana amewashangaza wengi waliokuwa wakiamini kuwa leo anakwenda kuomba kuinunua Yanga baada ya Mohammed Dewji maarufu kama Mo kutoa pendekezo la kununua Simba kwa asilimia 51 akitoa bilioni 20.

Pamoja na hivyo, Manji ameweka msisitizo katika suala la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwamba limekosea kuipa Azam FC nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho wakati Yanga ndiyo mabingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV