August 19, 2016Beki wa Yanga SC, Hassan Kessy aliyekosa penalti na kushuhudia Yanga ikifungwa kwa penalti 4-1 dhidi ya Azam katika mechi ya Ngao ya Jamii, juzi alijikuta akibaki na mshangao kwa kile alichofanyiwa na Wanayanga mara baada ya mchezo huo.

Kessy ambaye alijua anaweza kupata lawama nyingi kwa kukosa penalti katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, anasema kuwa alipigiwa simu nyingi na mashabiki wa Yanga waliokuwa wakimfariji.

"Naomba niwaombe radhi Yanga kwa kukosa penalti, ukweli ni kuwa ile mechi tulitakiwa kuimaliza mapema kwa kuwa tulitawala mchezo huo lakini ndiyo hivyo.
“Nashukuru mashabiki wa Yanga kwa kunipigia simu kujifariji na kunitia moyo baada ya kukosa penalti, niwaambie kuwa tupo pamoja," alisema Kessy na kuongeza:

“Siwezi kuzungumzia sana namna nilivyokosa lakini najisikia vibaya kwa kweli, inaniuma sana.”

Aidha, akizungumzia kuhusu kumwaga machozi mara kadhaa katika mchezo huo, Kessy alisema: “Nalia kwa sababu ya furaha kwani sikuamini kabisa kama ningeitumikia Yanga kwa sababu kila mtu anajua nini kinachoendelea dhidi yangu.


“Tangu nimetua Yanga nimekumbana na vizingiti vingi sana ambavyo vimenifanya nishindwe hata kucheza mechi za kimataifa ila naamini Mungu yupo na kila kitu kitakaa sawa,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV