August 21, 2016

Nguli wa soka kutoka Brazil, Ronaldo de Lima ametaja timu yake bora ‘dream team’ lakini jina la staa mmoja ambaye ni wajina wake halimo.
   
Ronaldo na Messi
De Lima maarufu kwa jina la Ronaldo wa Ukweli ambaye enzi zake alitamba katika timu za Real Madrid, Inter Milan na Barcelona aliwataja mastaa kadhaa kutoka taifa lake la Brazil katika kikosi hicho, Cafu na Roberto Carlos kisha akajichagua yeye mwenyewe na nguli mwenzake wa Brazil, Pele.

Katika kikosi hicho, staa wa Barcelona, Lionel Messi yumo ndani pia lakini nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo hakumtaja.
 
De Lima na Ronaldo

Katika kikosi hicho De Lima ambaye pia unaweza kumuita The Phenomenon amempanga Messi pembeni huku yeye na Pele wakisimama mbele.

Mbali na hapo De Lima amemtaja kiungo mkongwe Andrea Pirlo raia wa Italia ambaye kwa sasa anaichezea New York City FC ya Marekani.


Messi na Ronaldo de Lima

De Lima enzi zake

De Lima alivyo sasa

Inawezekana mtazamo huo wa De Lima ukawa mbaya kwa Ronaldo ambaye inajulikana kuwa huwa hapendi kushindwa au kushushwa thamani, katika mitandao ya kijamii na ile ya soka tayari mijadala imeanza juu ya uamuzi huo wa Mbrazili huyo na jinsi ambavyo Ronaldo Mreno atakavyopokea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV