August 14, 2016


Kocha wa Yanga, Hand van der Pluijm amesema wataendelea kuyafanyia kazi makosa ya kutomalizia vizuri ili wawe imara katika mechi yao ya mwisho ya Kundi A dhidi ya TP Mazembe.

Pluijm amesema kupoteza nafasi sana, kumewaathiri na kikosa pointi nyingi katika Kundi  A ambalo wao wanashika mkia katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho.

“Tunachotakiwa ni kushinda mechi ya mwisho, tutakuwa ugenini. Kikubwa ni kurekebisha mambo kadhaa na hilo la kupoteza nafasi,” alisema.

Yanga iliendelea na ugonjwa wake huo wa kupoteza nafasi baada ya kushindwa kufunga kila ilipopata nafasi katika mechi ya jana dhidi ya Mo Bejaia.


Yanga ilishinda mechi hiyo kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, lakini ingeweza kushinda hata kwa mabao manne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV