Nyota wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry ameanza rasmi kazi ya Kocha Msaidizi wa Ubelgiji.
Henry ametua jijini Brussels na kwenda moja kwa moja kwenye hoteli ya timu hiyo ambako alijitambulisha mwenyewe.
Baada ya hapo, alianza kazi akiwa chini ya Kocha Mkuu, Roberto Martinez, ambaye ni kocha wa zamani wa Everton.
Henry ambaye alianza kwa kuwa kocha wa vijana wa Arsenal kabla ya kuamua kufanya kazi ya uchambuzi, inaonekana sasa ameamua kuwa siriaz na kazi ya ukocha.
Kikosi hicho chenye mastaa kibao, kinajiandaa katika mechi dhidi ya Cyprus.
Kikosi hicho chenye mastaa kibao, kinajiandaa katika mechi dhidi ya Cyprus.
KIKOSI KAMILI CHA UBELGIJI:
MAKIPA: Courtois, Mignolet, Sels
WALINZI: Alderweireld, Kabasele, Lombaerts, J. Lukaku, Meunier, Vermaelen, Vertonghen
VIUNGO: De Bruyne, Defour, Dembele, Fellaini, Nainggolan, Witsel
WASHAMBULIAJI: Batshuayi, Benteke, Carrasco, E. Hazard, T. Hazard, R. Lukaku, Mertens, Mirallas, Origi
0 COMMENTS:
Post a Comment