Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog amewataka wachezaji wake kuzitumia nafasi watakazotengeneza ili kumaliza ukame.
“Ni kweli Omog amezungumza na wachezaji na kuweka msisitizo katika suala la kutumia nafasi kwa kuwa tulizipoteza nyingi sana,” kilieleza chanzo.
Simba imecheza mechi mbili za Ligi kuu Bara ikianza na ushindi wa mabao 3-1 dhidi Ndanda FC kabla ya sare ya bila kufungana dhidi ya JKT Ruvu.
Sare hiyo ndiyo imezua gumzo kwa kuwa Simba ilikosa nafasi nyingi za kufunga katika mechi hiyo iliyomaliza dakika 90 bila bao.
Hata katika mechi dhidi ya JKT Ruvu Simba pia ilipoteza nafasi nyingi za kufunga jambo ambalo Omog pia ameliona.
0 COMMENTS:
Post a Comment