August 21, 2016


Baada ya timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kumefanikiwa kusonga mbele katika Hatua ya Tatu kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa vijana ambayo itafanyika mwakani nchini Madagascar. Sasa itakutana na DR Congo.

Congo nayo imefanikiwa kusonga mbele baada ya kuitandika kuitwanga Namibia kwa mabao 3-0.

Mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 16,17&18  na kurudiana Oktoba na kama itavuka hapo, maana yako itakuwa imefuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika.

Serengeti ambayo katika mchezo wa kwanza wa Hatua ya Pili ya kuwania kufuzu michuano hiyo ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Afrika Kusini, leo imefanikiwa kusonga Hatua ya Tatu ya kuwania kufuzu michuano hiyo baada ya kuifunga Afrika Kusini mabao 2-0 katika mchezo wa marudio uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.   

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic