August 3, 2016


Kikosi cha Simba chini ya Kocha Joseph Omog kimeanza kuonja uchungu wa kipigo baada ya kuchapwa bao 1-0 katika mechi ya kirafiki dhidi ya KMC ya Kinondoni katika mechi iliyochezwa mjini Morogoro, leo.

KMC

Mechi hiyo ni ya tatu kwa Simba iliyo kambini mjini humo na ilianza mechi zake za kirafiki kwa kuitwanga Polisi Moro kwa mabao 6-0, ikaitandika Burkina Faso 5-0 kabla ya kuiangukia Moro Kids kwa mabao 2-0.

Lakini leo, mambo yameonekana ni magumu kwa Simba ambayo imekutana na kipigo cha mabao hayo mawili kutoka kwa timu hiyo ya daraja la kwanza.

Bao la ushindi lilifungwa na Rashid Roshwa katika dakika ya 10 ya mchezo, lakini Simba ilipambana vilivyo lakini haikuweza kurudisha.


1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV