August 18, 2016


Uongozi wa Simba, umejipanga kuwasilisha barua kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ukipinga na kutaka maelezo kuhusiana na uamuzi wa shirikisho hilo kumruhusu beki, Hassan Kessy kucheza mechi ya Ngao ya Jamii.

Kessy alicheza mechi hiyo wakati Yanga ikiivaa Azam FC na kupoteza kwa mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 za sare ya 2-2.

Kessy ambaye alikosa penalti katika mchezo huo, ikiwa ni penalti yake ya kwanza katika mechi ya kwanza Yanga, ana mgogoro wa usajili kwa kuwa Simba imesema alisajiliwa wakati akiwa bado na mkataba na Simba.

“Kweli kuna juhudi zinafanywa na barua inaweza kuwasilishwa TFF leo, Simba tunataka kupata ufumbuzi wa jambo hilo,” kilieleza chanzo.


2 COMMENTS:

  1. Kweli hii nchi ina mambo ya ajabu, kila siku vituko, chama hiki cha kisiasa kina haki zaidi ya kile, MKoa huu una haki zaidi ya ule, mara timu hii ina haki zaidi ya zile. Mchezaji kawekewa pingamizi kwa mujibu wa sheria ya usajili, inayoruhusu mchezaji kuwekewa pingamizi, kabla pingamizi halijapatiwa ufumbuzi kisheria anaruhusiwa kucheza mchezo unaotambulika na TFF. Kamwe soka halitaendelea, nani alishaendelea bila kuzingatia nakuheshimu utaratibu, kanuni na sheria?

    ReplyDelete
  2. Kanuni za Fifa zinamlinda mchezaji zaidi kwa sababu club zinawakomoa wachezaji, ndio maana Okwi aliruhusiwa kusajili villa wakati ana mgogoro na Etoil du sahel

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV