August 9, 2016

MAVUGO
Klabu ya Vital’O ya Burundi imesema imetuma jina la mshambuliaji Laudit Mavugo kwenye Shirikisho la Soka la Burundi kama sehemu ya usajili wake.

Vital’O imesisitiza kuwa Mavugo bado ni mchezaji wake na inashangazwa kuona amesajiliwa na Simba.

Mtandao wa klabu hiyo unaendelea Mavugo bado ana mkataba na Vital’O na aliondoka Burundi akienda kufanya majaribio Ufaransa.

“Amekwenda kufanya majaribio Ufaransa kwa ruhusa ya klabu. Baada ya kurejea baadaye tumeambiwa yuko Tanzania na amesajiliwa na Simba,” umefafanua mtandao huo wa mashabiki wa klabu hiyo.

Hata hivyo, Simba tayari imempa Mavugo mkataba wa miaka miwili kuanza kuitumikia na tayari amechota nyoyo za mashabiki wa Simba.

Mavugo alifunga bao moja na kutengeneza moja wakati Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mechi ya kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana maalum kwa ajili ya kusherekea Simba kutimiza miaka 80 katika Simba Day.


2 COMMENTS:

  1. Yaan ww jinga kabisa chanzo cha habari yako mtandao wa mashabiki alafu mwenyew unakaa unaandika, naona anawastua sana mavugo sasa afadhar muda huo mngeenda kukaa kujadil mlichokiamua kuhusu club yenu kama kina mantik badala ya kuandika upupu huku.

    ReplyDelete
  2. Usajili wa Bongo siku zote ni sarakasi tu.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV