August 10, 2016


Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga, ametamka kuwa uongozi wa Simba umemharibia mipango yake baada ya kuwachukua nyota wake muhimu waliong’ara na timu hiyo msimu uliopita na kumuachia mapengo.

Mayanga aliyepokea mikoba ya Mecky Maxime katika kuinoa timu hiyo, amesema hayo mara baada ya Simba kuwanasa nyota mahiri wa Mtibwa ambao ni Mzamiru Yassin, Shiza Kichuya na Mohammed Ibrahim waliokuwa wanafanya vizuri na kikosi hicho msimu uliopita.

Mayanga amesema mpaka sasa bado anatafuta njia mbadala ya kuweza kutatua tatizo la kiungo ndani ya timu yake ambalo linamuumiza kichwa kwa kuwatengeneza nyota wapya ambao watakuja kuziba nafasi za wachezaji hao.


“Timu yangu ipo vizuri kila sehemu isipokuwa kwenye eneo la kiungo ndiyo kuna shida kwa sababu tumepoteza nyota kadhaa ambapo sasa nina kazi ya kutengeneza waliopo kwa ajili ya kuziba mapengo yao kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi,” alisema Mayanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV