August 28, 2016

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amemtaka kiungo mshambuliaji wake, Mesut Ozil kuhakikisha anafunga mabao mengi msimu huu.

Kauli hiyo ameitoa baada ya mchezaji huyo kuwemo katika kikosi cha Arsenal kilichoibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Watford, jana Jumamosi katika Premier League.
Mchezo huo ulikuwa kwa kwanza kwa Ozil tangu arejee klabuni hapo akitokea kwenye mapumziko ya msimu, ambapo amekuta timu yake ilikuwa na pointi moja katika michezo miwili kabla ya mchezo wa jana.

"Nafikiri tumeona uwezo wake, anao uwezo wa kutoa asisti na kufunga pia, anatakiwa kuendelea kufunga mabao mengi ili kutoa hamasa kwa wenzake na kutoa asisti nyingi,” alisema Wenger.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV