September 5, 2016

KIPA AISHI MANULA
Wachezaji Shomari Kapombe, Aishi Manula na David Mwantika wameungana na kikosi cha Azam FC kilichopo mjini Mbeya.

Wachezaji hao wameungana kwa nyakati tofauti na kikosi hicho wakitokea nchini Nigeria ambako walikwenda kuitumikia timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa inawavaa Nigeria.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amethibitisha wachezaji hao kujiunga na wenzao.

“Tayari wameungana na wenzao, hivyo kikosi sasa kimekamilika na kipo kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Prisons,” alisema.


Azam FC itaanza kwa kuwavaa Prisons Jumatano, kabla ya kukutana na Mbeya City. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV