Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho anaamini timu yake ilikuwa ikitakiwa upata penalti mbili katika mchezo wa jana dhidi ya Manchester City.
Mourinho amemlalamikia mwamuzi wa mchezo huo, Mark Clattenburg kwa kutoipa penalti timu yake na kutomtoa nje kwa kadi nyekundu kipa wa Manchester City, Claudio Bravo katika mchezo huo ambao timu yake ilifungwa mabao 2-1.
Bravo alionekana akimchezea faulo nahodha wa Mam United, Wayne Rooney ambapo mshambuliaji huyo alilala kwa maumivu huku akishika mguu wake lakini mwamuzi aliruhusu mchezo uendelee.
Tukio la pili ambalo linallamikiwa ni mpira wa krosi uliopigwa na beki United, Antonio Valencia na kumgonga mkononi beki wa City, Nicolas Otamendi ndani ya eneo la 19 la City.
"Ni penalti halali na kadi nyekundu kwa Bravo. Hata ile faulo ni penalti pia kwa kuwa aliona mpira ulivyokuwa ukija, akageuka na kuweka mkono.
“Mwamuzi ni binadamu kama sisi, kuna wakati huwa hawafikirii mara mbili.
“Tuliadhibiwa kutokana na maamuzi yake mabaya hasa kipindi cha pili, lakini hilo ndilo soka,” alisema Mourinho .
Jose Mourinho |
Rooney akilalamika kwa Mark Clattenburg |
Bravo na Rooney ilivyokuwa. |
Bravo na Rooney |
Valencia akipiga faulo inayolalamikiwa na Mourinho. |
Bravo alionekana akimchezea faulo nahodha wa Mam United, Wayne Rooney ambapo mshambuliaji huyo alilala kwa maumivu huku akishika mguu wake lakini mwamuzi aliruhusu mchezo uendelee.
Tukio la pili ambalo linallamikiwa ni mpira wa krosi uliopigwa na beki United, Antonio Valencia na kumgonga mkononi beki wa City, Nicolas Otamendi ndani ya eneo la 19 la City.
"Ni penalti halali na kadi nyekundu kwa Bravo. Hata ile faulo ni penalti pia kwa kuwa aliona mpira ulivyokuwa ukija, akageuka na kuweka mkono.
“Mwamuzi ni binadamu kama sisi, kuna wakati huwa hawafikirii mara mbili.
“Tuliadhibiwa kutokana na maamuzi yake mabaya hasa kipindi cha pili, lakini hilo ndilo soka,” alisema Mourinho .
0 COMMENTS:
Post a Comment